Inhaltspezifische Aktionen

Kiswahili

Hatua ya 1: Pakua programu

Njia rahisi zaidi ya kuwa raia mwanasayansi na kuwasilisha uchunguzi wako mwenyewe ni kwa kutumia programu ya HydroCrowd. Programu inaweza kutumika kuangalia uchunguzi (unaoitwa ‘spots’ katika programu) yaliyowasilishwa na watu wengine katika HydroCrowd na unaweza kuwasilisha uchunguzi wako mwenyewe. Pakua programu bila malipo kwa smartphone yako:

Hatua ya 2: Sajili (si lazima)

Hasa ikiwa unapanga kuwasilisha uchunguzi mara nyingi au kupita vituo vingi wakati wa kutembelea moja ya maeneo yetu ya utafiti, inafaa kutengeneza akaunti ya mtumiaji. Ikiwa ungependa kuwasilisha data bila kukutambulisha, unaweza kuruka hatua hii.

Ikiwa hutumii akaunti ya mtumiaji, utaulizwa ikiwa ungependa kutuma uchunguzi bila kujulikana au kama ungependa kuuhifadhi uchunguzi wako. Chagua 'Send anonymously' (Tuma bila kujulikana).

  • Fungua programu ya HydroCrowd kwenye simu janja yako.
  • Unapoulizwa, tafadhali ruhusu programu kufikia eneo lako.
  • Baada ya kupitia utangulizi, bonyeza 'Register' (Jisajili).
  • Toa maelezo yanayohitajika. Kisha ubofye kwenye 'Register' (Jisajili) ili kukamilisha usajili na SpotterOn.

  • Baada ya usajili, unaweza kugeuza wasifu wako wa mtumiaji HydroCrowd kadri utikavyokufaawa. Hii ni hiari. Bonyeza ‘Save’ (Hifadhi) unapomaliza.
  • Mara ya kwanza unapotaka kuongeza eneo jipya au kuongeza uchunguzi kwenye eneo lililopo, utaulizwa jukumu lako la mtumiaji ni nini. Chagua 'Regular user’ (Mtumiaji wa kawaida).

Karibu Crowd! Uko tayari kuwasilisha uchunguzi wako!

Hatua ya 3: Itambue program

Hebu tuanze kwa kuangalia vitufe muhimu zaidi kwa mtumiaji.

Hatua ya 4: Tazama kituo

Ili kuangalia uchunguzi wa awali, bofya kwenye kituo kwenye ramani.

Hatua ya 5: Pakua kituo kwa matumizi wakati huna mtandao

Katika vituo vingi, hakuna mtandao wa simu za mkononi au WiFi. Kwa matumizi bora zaidi, unaweza kupakua kituo kwa matumizi wakati huna mtandao. Utaweza kuhifadhi uchunguzi wako wakati huna mtandao na uwasilishe baadaye ukiwa umerudi mahali penye mtandao.

  • Tafuta kituo unachopanga kukitembelea kwenye ramani na ubofye juu yake, ili uone uchunguzi wa mwisho.
  • Fungua menyu ya kituo.
  • Chagua 'Download Spot to device’ (Pakua Kituo kwenye kifaa).

Mduara wa kijani wenye mshale mweupe unaoelekea chini unapaswa kuonekana, kwenye kituo kilichopakuliwa. Sasa kituo kitaonekana kila wakati, hata kama huna mtandao

Unaweza kupata vituo ulivyopakua kwenye menyu ya programu chini ya ‘Offline maps & spots’ (Ramani za nje ya mtandao na vituo).

Hatua ya 6a: Wasilisha uchunguzi kutoka kituo cha hali ya hewa

Ikiwa uko katika kituo cha hali ya hewa na una mtandao au umepakua kituo kwa matumizi ya nje ya mtandao (nenda Hatua ya 5), fuata maelekezo haya.

  • Bofya kwenye kituo kilicho karibu zaidi na eneo lako kwenye ramani au chagua kituo kutoka kwenye orodha yako ya vituo vya nje ya mtandao, ikiwa umepakua kituo kwa matumizi ya nje ya mtandao.
  • Bonyeza kitufe cha KUJUMLISHA ili kuongeza uchunguzi wako mwenyewe.
  • Bonyeza kitufe cha kamera kupiga picha ya uchunguzi wako. Picha inapaswa kuonyesha wazi kipima unyevunyevu, kipima joto na kipima mvua. Kubali picha na ubonyeze ‘OK’ (Sawa).
  • Jibu maswali katika programu. Ikiwa ungependa maelezo zaidi, bofya kitufe cha ‘i’ kilicho upande wa kulia wa swali. Hii inafanya kazi tu wakati una mtandao.
  • Iwapo kituo kimeharibika au hakifanyi kazi, tafadhali weka alama kwenye kisanduku ‘The weather station is damaged’ (Kituo cha hali ya hewa kimeharibika) na utujulishe tatizo ni nini.
  • Tumia kisanduku cha maandishi kwenye ‘Would you like to share anything else?’ (Je, ungependa kushiriki kitu kingine chochote?) kuwasilisha maoni yoyote kuhusu kituo au mradi.
  • Bofya kwenye 'Save’ (Hifadhi) ili kuwasilisha uchunguzi wako moja kwa moja kama uko mtandaoni. Ikiwa huna mtandao, utapata onyo litakalokuuliza ikiwa ungependa kuhifadhi eneo hilo kwa muda. Bofya ‘OK’ (Sawa) na ufuate maelekezo katika Hatua ya 7 ili kuiwasilisha utakaporejea mtandaoni.

Hatua ya 6b: Wasilisha uchunguzi kutoka kituo cha maji

Ikiwa uko kwenye kituo cha maji na una mtandao au umepakua kituo kwa matumizi ya nje ya mtandao (nenda Hatua ya 5), fuata maagizo haya.

  • Bofya kwenye kituo kilicho karibu zaidi na eneo lako kwenye ramani au chagua kituo kutoka kwenye orodha yako ya vituo vya nje ya mtandao, ikiwa umepakua kituo kwa matumizi ya nje ya mtandao.
  • Bonyeza kitufe cha KUJUMLISHA ili kuongeza uchunguzi wako mwenyewe.
  • Bonyeza kitufe cha kamera kupiga picha ya uchunguzi wako. Picha inapaswa kuonyesha wazi kipimo cha kiwango cha maji (Rula) kwenye mto. Hakiki picha na ubonyeze ‘OK’ (Sawa).
  • Jibu maswali kuhusu kiwango cha maji kwenye programu. Ikiwa ungependa maelezo zaidi, bofya kitufe cha ‘i’ kilicho upande wa kulia wa swali. Hii inafanya kazi tu wakati una mtandao.
  • Tumia jagi kukusanya maji kutoka mtoni. Fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye ishara ili kupima topetope kwenye maji. Kisha jibu maswali kuhusu rangi ya maji na topetope katika programu.
  • Iwapo kituo kimeharibika au hakifanyi kazi, tafadhali weka alama kwenye kisanduku ‘The water station is damaged’ (Kituo cha maji kimeharibika) na utujulishe tatizo ni nini.
  • Tumia kisanduku cha maandishi kwenye ‘Would you like to share anything else?’ (Je, ungependa kushiriki kitu kingine chochote?) kuwasilisha maoni yoyote kuhusu kituo au mradi.
  • Bofya kwenye ‘Save’ (Hifadhi) ili kuwasilisha moja kwa moja uchunguzi wako kama uko mtandaoni. Ikiwa huna mtandao, unapata onyo litakalokuuliza ikiwa ungependa kuhifadhi eneo hilo kwa muda. Bofya ‘OK’ (Sawa) na ufuate maelekezo katika Hatua ya 7 ili kuiwasilisha utakaporejea mtandaoni.

Hatua ya 6c: Wasilisha Photo Note

Je, unaona jambo lisilo la kawaida au la kuvutia na linalohusiana na hali ya hewa au maji? Wasilisha jambo hilo kupitia Photo Note (Dondoo za Picha)!

  • Bofya kwenye kitufe cha KUJUMLISHA chini ya skrini ili kuongeza kituo.
  • Angalia ikiwa eneo lako kwenye ramani ni sahihi.
  • Chagua 'Photo Note’ (Dondoo za Picha)
  • Piga picha au pakia picha ya uchunguzi wako na utoe maelezo mafupi.
  • Bofya kwenye 'Save’ (Hifadhi) ili kuwasilisha uchunguzi wako moja kwa moja kama uko mtandaoni. Ikiwa huna mtandao, unapata onyo litakalokuuliza ikiwa ungependa kuhifadhi eneo hilo kwa muda. Bofya ‘OK’ (Sawa) na ufuate maelezo katika Hatua ya 7 ili kuiwasilisha utakaporejea mtandaoni.

Iwapo ungependa kutusaidia kuboresha mradi au programu, chagua ‘Yes’ (Ndiyo) katika swali ikiwa ungependa kuwasilisha uzoefu wako na HydroCrowd, na ujibu maswali manne ili kuunda kitambulisho chako cha kipekee kisichokutambulisha. Unahitaji kufanya hivi mara moja tu, na sio baada ya kila uchunguzi unaotuma.

Hatua ya 7: Wasilisha uchunguzi wako baadae

Ikiwa ulichukua uchunguzi ukiwa huna mtandao, fuata hatua zinazofuata ili kuwasilisha uchunguzi wako utakaporejea sehemu yenye mtandao.

  • Fungua menyu ya programu na uchague ‘Waiting spots’ (Sehemu ya kusubiri).
  • Bonyeza uchunguzi unaotaka kuwasilisha.
  • Bofya kwenye ‘Save’ (Hifadhi) chini ya skrini ili kuwasilisha uchunguzi wako.

Hatua ya 8: Piga picha na uwasilishe baadaye

Ikiwa utapita karibu na kituo, lakini ukawa huna programu au hakuna mtandao na hukupakua kituo hicho kwa matumizi ya nje ya mtandao, unaweza kupiga picha ya uchunguzi wako na kuiwasilisha baadaye kwa kutumia programu au kupitia www.spotteron.com/hydrocrowd.

  • Piga picha ya uchunguzi wako inayofanana na picha iliyoonyeshwa hapa.
  • Unaporejea mtandaoni, fungua programu au nenda kwa www.spotteron.com/hydrocrowd. Chagua kituo kwenye ramani na ubofye kitufe cha KUJUMLISHA ili kuwasilisha uchunguzi wako.
  • Ili kuwasilisha picha yako, bofya kwenye kitufe cha picha na uchague picha kwenye simu yako. Inabidi uruhusu ruhusa ya programu kufikia faili la picha kwenye simu yako. Chagua picha na ubonyeze ‘OK’ (Sawa).
  • Dirisha ibukizi litaonekana, likikuuliza ikiwa unataka kuleta taarifa za picha yako. Chagua ‘Date/time’ (Tarehe/saa) na ubonyeze 'OK' (Sawa).
  • Jibu maswali yaliyosalia na ubofye kwenye ‘Save’ (Hifadhi) ili kuwasilisha uchunguzi wako.


Kwa habari zaidi kuhusu mradi na video muhimu kuhusu jinsi ya kutumia programu, tufuate kwenye mitandao ya kijamii: